Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA
Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Karim Mandonga amefanikiwa kushinda mkanda wa Ubingwa wa PST kufuatia mkuchapa kwa pointi Kenneth Lukyamuzi kutoka Uganda.
Katika pambano hilo ambalo limepigwa kwa raundi nane kwenye uzani wa Super Middle, Mandonga amefanikiwa kumchapa mpinzani wake huyo ambaye hata hivyo hakuwa tayari kukubali matokeo hao kwa kusisitiza kutaka pambano la marudiano.
Mbali ya Mandonga kushinda pambano hilo ambalo limepigwa hapa kwenye Uwanja wa Kasarani jijni Nairobi, mabondia wengine wa Tanzania waliofanikiwa kushinda ni Fatma Yazidu ambaye amemchapa kwa pointi Consalata Musanga lakini Hassan Ndonga naye ametandika kwa pointi Nick Otieno wa Kenya.
Zawadi Kutaka yeye amepoteza kwa pointi mbele ya Plaxedus Odouri huku George Bonabucha akipoteza mbele ya Albert Kimario wa Kenya.
No comments:
Post a Comment