Lomalisa Afunguka haya kuhusu ubora wake kwasasa - EDUSPORTSTZ

Latest

Lomalisa Afunguka haya kuhusu ubora wake kwasasa

 

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA

Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Kwa sasa beki wa kushoto wa Yanga, Joyce Lomalisa gari limewaka kutokana na kasi aliyonayo, tofauti na alivyoanza mara aliposajiliwa mwanzoni wa msimu huu


Lomalisa alitua Yanga akitokea FC Onze Bravos do Maquis ya Angola na kuanza kwa kusuasua lakini kwa sasa anakimbiza kiasi cha kushangaza


Lomalisa amebainisha kuwa ubora wa kikosi cha Yanga kikiwa na malengo ndio siri iliyombeba na kumfanya aingie kwenye mfumo na kuonekana kuwa bora, huku akikiri anajiona kuwa bora zaidi kutokana na morali nzuri ya wachezaji anaocheza nao


"Ubora wangu unatokana na namna timu inavyocheza ambayo inanilazimisha na mimi niingie kwenye mfumo kwa kufuata kile wanachokitaka nashukuru nimefanikiwa kwenye hilo," alisema Lomalisa 


"Yanga ina wachezaji wengi wenye malengo sawa, hivyo ili kuweza kuingia kikosini timu itakulazimisha nawe kuendana na kile wao wanachokitaka nafurahi kwa muda nilioingia ndani ya timu hii nimeweza kuelewana na wachezaji wenzangu ikiwa ni pamoja na kuingia kwenye mfumo wa kocha"


Akizungumzia michuano ya Kimataifa, Lomalisa alisema malengo yao kama timu ni kuhakikisha wanatinga nusu fainali baada ya kufanikiwa kufuzu robo, akiamini wakipambana wanaweza kutoboa na kufika mbali zaidi


"Yanga ina kikosi kizuri imefika kwenye hatua ambayo ni mwanzo mzuri kwetu kuendeleza juhudi tulizoanzisha ili kufikia lengo hilo linawezekana kilichobaki ni benchi la ufundi kufanya kazi yao na wachezaji kufanya kwa vitendo"


"Benchi la ufundi, wachezaji na viongozi wote unatakiwa kuwa na lengo moja ili kuweza kufanya mambo ambayo yataifanya timu kuwa bora na ya ushindani kama tulivyoanza ili tumalize pia kwa ubora"


Alisema mchezo uliobaki ili kukamilisha makundi bado wanauchukulia kwa umuhimu zaidi ili kuhakikisha wanamaliza kundi kwa kuongoza na kuweka rekodi ambayo anaamini itadumu kutokana na timu hiyo kutoweza kufikia mafanikio hayo kwa muda.


"Aprili 2, tutakuwa ugenini kuwakabili TP Mazembe ni mchezo ambao hatutarajii mteremko tunatakiwa kujiandaa vizuri ili kwenda kusaka rekodi ya kushinda ugenini na kupata pointi tatu ambazo zitatuimarisha kileleni kwenye kundi D." alisema Lomalisa


Mwanaspoti



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz