Tetesi za usajili barani ulaya Leo Jumatatu March 20 - EDUSPORTSTZ

Latest

Tetesi za usajili barani ulaya Leo Jumatatu March 20

Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA

Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
 

Aston Villa wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 29, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo huko Inter Milan akitokea Chelsea. (Todo Fichajes – in Spanish)


Manchester United wako tayari kumuuza nahodha na beki wa kati wa England Harry Maguire, 30, na mlinzi wa Uswisi Victor Lindelof, 28, msimu huu. (Football Insider)


Meneja Jurgen Klopp anataka Liverpool kumpa kiungo mkongwe wa Uingereza James Milner, 37, mkataba mpya. (Football Insider)


Chelsea wana nia ya kumnunua kipa wa Inter Milan na Cameroon Andre Onana, 26, msimu wa joto. (InterLive, via Fichajes - in Spanish)


Arsenal wanataka kumsajili beki wa kulia wa Galatasaray Mfaransa Sacha Boey, 22. (Aksam - in Turkish)


Kiungo mshambuliaji wa Ujerumani Marco Reus, 33, anataka kusalia Borussia Dortmund, ambako ni nahodha, hadi mwisho taaluma yake . (Sky Germany - in German)


Chelsea na Newcastle wote wanamfuatilia mshambuliaji wa zamani wa Manchester City Brahim Diaz. Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa sasa yuko kwa mkopo huko AC Milan kutoka Real Madrid lakini anaweza kupatikana mwishoni mwa msimu huu. (Sun)


Tottenham wanaweza kufufua nia yao ya kumnunua beki wa kati wa Napoli na Korea Kusini Kim Min-jae, 26, msimu huu. (Football Insider)


Everton watamnunua mshambuliaji wa West Ham kutoka Jamaica Michail Antonio, 32, msimu wa joto, iwapo wataepuka kushushwa daraja. (Sun)


Kiungo wa kati wa Ghana Mohammed Kudus, 22, anatumai kusalia Ajax hadi mwisho wa msimu huu licha ya Manchester United, Arsenal na Liverpool kumtaka. (De Telegraaf, via 90min)


Besiktas wanajiandaa kuanzisha kipengee cha kununu kununua katika mkataba wao wa mkopo wa beki wa West Ham kutoka Congo Arthur Masuaku, 29. (Fanatik, via Inside Futbol)


Kocha wa zamani wa Everton Frank Lampard yuko tayari kwa nafasi yake nyingine ya ukocha, karibu miezi miwili tangu atimuliwe na The Toffees. (Sun)


BBC



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz