Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Nyota saba wa Simba wamejumuishwa katika vikosi vya timu za Taifa ambazo mwishoni mwa wiki watashuka dimbani kusaka tiketi za kufuzu michuano ya Afcon 2023
Aishi Manula, Beno Kakolanya, Mzamiru Yassin, Hennock Inonga, Clatous Chama, Peter Banda na Saido Ntibazonkiza wameruhusiwa kujiunga na timu za Taifa
Wachezaji ambao hawana majukumu ya timu za Taifa wamepewa mapumziko ya siku chache kabla ya kurejea mazoezini kujiandaa na ratiba ya mechi zinazofuata
March 31 Simba itakuwa ugenini Morocco kukamilisha ratiba ya hatua ya makundi ligi ya mabingwa kwa mchezo dhidi ya Raja Casablanca
Mechi mbili dhidi ya Ihefu Fc zitafuata. Wataanza na mchezo wa kombe la FA ambao utapigwa kati ya April 03/06 na baadae kusafiri mkoani Mbeya kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ambao utapigwa dimba la Ihefu, April 08
Baada ya mchezo huu Simba itarejea jijini Dar es salaam tayari kwa mchezo dhidi ya Yanga ambao utapigwa April 16
No comments:
Post a Comment