Hizi hapa timu zilizo tinga Robo fainali ligi ya mabingwa mpaka sasa - EDUSPORTSTZ

Latest

Hizi hapa timu zilizo tinga Robo fainali ligi ya mabingwa mpaka sasa


 Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA

Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Mechi za mwisho kuhitimisha hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika zinatarajiwa kupigwa mwisho mwa mwezi huu March 31 na April 01


Simba ni miongoni mwa timu saba ambazo tayari zimejihakikishia tiketi ya kucheza robo fainali


Wydad Athletic na JS Kabylie kutoka kundi A nao wamefuzu robo fainali mechi za mwisho zitaamua timu ipi itamaliza kinara wa kundi timu zote zikiwa na alama 10


Mamelod Sundowns tayari imefuzu kundi B wakati Al Ahly na Al Hilal zitachuana kwenye mchezo wa mwisho kuamua timu ipi inaingia robo fainali sambamba na Sundowns


Al Hilal wanahitaji alama moja tu wakati Al Ahly wanahitaji ushindi katika mchezo huo ambao watakuwa nyumbani


Kundi C ni Raja Casablanca na Simba timu hizo zitakutana kwenye mchezo wa mwisho kwa ajili ya kukamilisha ratiba tu


Raja wamemaliza vinara wa kundi wakati Simba wakimaliza nafasi ya pili


Kundi D ni Esperance na CR Belouisdad zilizofuzu robo fainali, mechi za mwisho zitaamua ni timu ipi itamaliza kinara wa kundi


Esperance wana alama 10 wakati CR Belouisdad wana alama tisaDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz