Haya hapa Matokeo ya Mechi ya Barcelona vs Real Madrid hapo jana - EDUSPORTSTZ

Latest

Haya hapa Matokeo ya Mechi ya Barcelona vs Real Madrid hapo jana

Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA

Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Barcelona wamepiga hatua kubwa kuelekea ubingwa wa Liga baada ya Franck Kessie kufunga bao la ushindi dakika za lala salama na kuizamisha Real Madrid 2-1 kwenye El Clasico usiku wa kuamkia leo

Real Madrid walitangulia kufunga baada ya Araujo kujifunga katika harakati za kuokoa krosi ya Vinicius Junor lakini Sergio Roberto akaisawazishia Barcelona kabla ya mapumziko

Real Madrid walifunga bao la pili dakika 10 kabla ya mchezo kumalizika lakini maamuzi ya VAR yalifuta bao hilo mfungaji Asensio akiwa ametokea eneo la kuotea

Ulikuwa mchezo ambao Barcelona walionyesha kuzitaka alama zote tatu, walitengeneza nafasi nyingi kuliko wapinzani wao

Ni ushindi ambao unaiweka Fc Barcelona kileleni mwa msimamo wa La Laiga kwa tofauti ya alama 12 dhidi ya Real Madrid inayoshika nafasi ya pili

Barcelona wamekusanya alama 68 katika mechi 26 wakati Real Madrid wana alama 56Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz