Mabosi wa Yanga waamua kusafiri na Timu kwenda Dr Congo - EDUSPORTSTZ

Latest

Mabosi wa Yanga waamua kusafiri na Timu kwenda Dr Congo

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 

Katika kuonyesha kuwa Yanga 'inautaka' kwelikweli mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe ambao utapigwa Jumapili, April 02,  msafara ulioondoka mapema leo umewajumuishwa vongozi waandamizi wa Yanga na GSM


Wajumbe wawili wa Baraza la Wadhamini Abbas Tarimba na Geofrey Mwambe wako katika msafara huo ambao pia yumo 'bosi kubwa' Ghalib Said Mohamed (GSM)


Rais wa Yanga Injinia Hersi Said yeye ameongoza safu ya uongozi, msafara mzima ukiwa na takribani watu 44


Ni mara chache sana kumuona GSM akisafiri na timu, unapoona kafanya hivyo basi fahamu huko aendako kuna jambo kubwa!


Yanga imedhamiria kuweka rekodi ya kuvuka hatua ya robo fainali ambayo tangu mfumo mpya wa mashindano ta CAF ulipoanza kutumika mwaka 2016, hakuna timu ya Tanzania ambayo imewahi kuvuka hatua hiyo iwe ligi ya mabingwa au kombe la Shirikisho


Hesabu za Yanga ni kumaliza nafasi ya kwanza kwenye kundi D nafasi ambayo mpaka sasa bado wanaishikilia


Wananchi wanahitaji kushinda mchezo dhidi ya TP Mazembe ili kujiweka katika nafasi nzuri huku wakisubiri matokeo ya mchezo kati ya US Monastir dhidi ya Real Bamako ambao utapigwa saa 4 usiku. Mechi ya TP Mazembe dhidi ya Yanga itapigwa saa 10 jioni


Yanga imefunga mabao mengi kuliko Monastir na pia wana uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa wakiizidi Monastir GD 1


Kama Yanga watashinda hata bao moja dhidi ya TP Mazembe, basi US Monastir watahitaji kushinda angalau mabao matatu kuipiku Yanga kileleni


Hivyo Wananchi watahitaji kupata ushindi wowote ingawa wakifunga zaidi ya mabao mawili itawaweka katika nafasi nzuri zaidi ya kumaliza kileleniDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz