Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mwekezaji wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' amesema bado ndoto yake kubwa ni kuiona Simba ikitwaa taji la ligi ya mabingwa barani Afrika
Mo ambaye tangu aanze kuwekeza Simba, katika kipindi chake cha miaka mitano, Simba imefanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya CAF mara nne
Simba imecheza robo fainali ya ligi ya mabingwa mara tatu na kombe la Shirikisho mara moja
Mo amesema Simba tayari ina mataji 22 ya ligi kuu, hivyo angependa zaidi kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa
Aidha Mo ameeleza kufurahia na ushindani ulioletwa na Yanga kwenye ligi ya ndani akiamini hiyo ni chachu kwao kujiimarisha na kuifanya ligi kuwa bora zaidi
"Nawapongeza Yanga kuleta ushindani mkubwa ndani ya Ligi wamefanya kazi kubwa, mpira usipokuwa na ushindani hauna ladha kwa hilo lazma niwapongeze Yanga na nawatakia kila La kheri kwenye mashindano Confederation na wao pia wafanikiwe ili timu nne ziendelee kushiriki kwenye mashinda haya makubwa"
"Mimi naona sisi (Simba) lazima tujipange upya ili tuweze sio tu kwenye Ligi. Huku kwenye ligi tumeshashinda mara 22 kwangu ni muhimu zaidi kushinda Champions League Africa," alisema Mo katika mahojiano na Global TV Online
No comments:
Post a Comment