Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Ni mchezo wa kukamilisha ratiba kwa sababu Raja na Simba zimefuzu hatua ya robo fainali kundi C, Raja ikimaliza nafasi ya kwanza na Simba ikishika nafasi ya pili
Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira anakiandaa kikosi chake bila ya nyota wake saba ambao wako kwenye majukumu ya timu za Taifa
Aidha katika mchezo huo, Simba pia itawakosa wachezaji wake Mohammed Hussein 'Tshabalala' na Kibu Denis wanaotumikia adhabu ya kadi mbili za njano
Tshabalala alionyeshwa kadi za njano katika mechi zote mbili dhidi ya Horoya Ac, wakati Kibu alionyeshwa kadi za njano katika michezo dhidi ya Vipers Fc (Ugenini) na Horoya Ac
Huenda Gadiel Michael akapata nafasi ya kucheza mechi yake ya kwanza ya ligi ya mabingwa msimu huu katika mchezo dhidi ya Raja wakati Robertinho ana wachezaji wengi ambao anaweza kuwatumia katika nafasi ya Kibu
Robertinho huenda akalazimika kufanya mabadiliko ya kikosi chake ili kuhakikisha anakuwa kikosi imara katika mchezo wa robo fainali
Baadhi ya nyota wana kadi za njano ambapo kama watapata kadi ya pili katika mchezo huo watakosa mechi ya kwanza ya robo fainali
Wachezaji hao ni Shomari Kapombe, Joash Onyango, Hennock Inonga, Mzamiru Yassin, Saido Ntibazonkiza, Pape Ousmane Sakho, John Bocco na Moses Phiri
No comments:
Post a Comment