Tanzania dimbani Leo dhidi ya Uganda - EDUSPORTSTZ

Latest

Tanzania dimbani Leo dhidi ya Uganda

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA

Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA

Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
 
Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo majira ya saa 11 itashuka dimba la Suez Canal huko Ismailia, Misri kuikabili Uganda Cranes katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Afcon 2023


Uganda ndio wenyeji wa mchezo huo ambao walilazimika kuupeleka Misri baada ya CAF kukataa viwanja vya Uganda kwa kukosa sifa


Hii ni nafasi ya adimu kwa Tanzania kusaka ushindi katika mchezo ambao ni kama timu zote zitakuwa ugenini


Baada ya Niger kuchapwa mabao 2-1 na Algeria hapo jana, timu itakayoshinda leo itapanda mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi F


Itakuwa mechi ya kwanza kwa kocha Adel Amrouche ambaye alikabidhiwa majukumu ya kuinoa Stars hivi karibuni


Amrouche amesema pamoja na vijana wake kupata muda mfupi wa kufanya mazoezi ya pamoja, wako tayari kwa mchezo huo ambao dhamira yao ni kusaka ushindi


Mchezo wa marudiano utapigwa jijini Dar es salaam siku ya Jumanne, March 28 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Mechi Itakuwa live kupitia app hii bofya hapa kuidownload ili uweze kuitazama mechi Mubashara kupitia simu YakoDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz