Je ni kweli yanga wamefungiwa kutofanya usajili haya hapa majibu ya kocha Luc Eymael anaye idai Yanga - EDUSPORTSTZ

Latest

Je ni kweli yanga wamefungiwa kutofanya usajili haya hapa majibu ya kocha Luc Eymael anaye idai Yanga

 

Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA

Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Kocha wa zamani wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa timu hiyo haijafungiwa kusajili madirisha matatu na Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) kwa kosa la kuchelewa kumlipa madai yake kama ilivyoripotiwa na chombo kimoja cha habari mapema jana


Eymael amebainisha kuwa uamuzi uliotolewa na FIFA ni kuitaka Yanga kulipa madai yake ili isikumbane na adhabu hiyo.


Kauli hiyo ya Eymael imekuja muda mfupi baada ya mtandao mmoja wa Afrika Kusini kudai kuwa Yanga imefungiwa kusajili kwa madirisha matatu kwa kosa la kutomlipa kocha huyo.


"Nadhani walioandika taarifa hiyo wameripoti kinyume. FIFA walitoa uamuzi na pande zote tumejulishwa kwamba Yanga wanatakiwa kunilipa stahiki zangu ndani ya siku 45 na iwapo wakishindwa kufanya hivyo, kuna adhabu kubwa zaidi watapewa ikiwemo ya kufungiwa kusajili," alisema


Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema taarifa hii imeibuliwa kwa nia ovu ya kuwavuruga mashabiki na wanachama wa Yanga kuelekea mchezo dhidi ya US Monastri ambao utapigwa Jumapili


Kamwe amesema suala la Eymael na Yanga sio geni na pande zote zimekuwa na mawasiliano Yanga ikiwa tayari imeshalipa sehemu ya deni hilo


"Kwa jinsi taarifa hii ilivyoripotiwa utaona hakuna nia njema kwa Yanga, lilikuwa ni suala la kufanya utafiti kidogo tu kijiridhisha na ukweli wa taarifa hiyo kabla ya kuisambaza kwenye mitandao ya kijamii"


"Imekuwa kawaida kila Yanga inapoelekea kwenye mchezo muhimu kuna jambo linatokea ili kutuondoa kwenye reli lakini sisi tunasema wameshindwa. Focus yetu ni mchezo dhidi ya Monastir," alisema Kamwe



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz