Hizi hapa timu zilizo tinga Robo fainali Europa League Jana - EDUSPORTSTZ

Latest

Hizi hapa timu zilizo tinga Robo fainali Europa League Jana

Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA

Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Usiku wa kuamkia leo Arsenal iliondoshwa kwenye ligi ya Europa kwa mikwaju ya penati 5-3 baada ya matokeo ya sare ya bao 1-1 katika mchezo uliopigwa kwa dakika 120


Changamoto ya mikwaju ya penati ilitumika kupata mshindi baada ya matokeo ya jumla kuwa 3-3. Timu hizo zilitoka 2-2 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Ureno


Granit Xhaka aiitanguliza Arsenal mapema lakini shuti la mbali la Pedro Goncalves liliirejesha Sporting mchezoni na kulazimisha dakika 30 za muda wa ziada


Kocha Mkuu wa Arsenal Mikel Arteta alifanya mabadiliko makubwa ya kikosi chake akiwapa mapumziko wachezaji wake muhimu


Arsenal imeweka nguvu kubwa kwenye kuwania ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza ambapo siku ya Jumapili watachuana na majirani zao kutoka jiji la London, Crystal Palace


Katika mechi nyingine Manchester United ilitinga robo fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-1 dhidi ya Real Betis


Man United walishinda 4-1 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Uingereza


Timu nyingine zilizotinga robo fainali ni Fayenoord, Sevilla, Juventus, B Leverkusen, Roma na Union St GilloiseDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz