Tetesi za usajili barani ulaya Leo Ijumaa February 17,2023 - EDUSPORTSTZ

Latest

Tetesi za usajili barani ulaya Leo Ijumaa February 17,2023

Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA

Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
 

Manchester United wako tayari kuwasilisha dau la kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Jude Bellingham, 19, kutoka Borussia Dortmund. (Telegraph - usajili unahitajika)


Newcastle United wanataka kumpa kipaumbele kiungo wa Leicester James Maddison msimu huu wa joto huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 akisemekana kutaka kucheza Ligi ya Mabingwa na kuwa mchezaji wa kawaida katika kikosi cha England. (The I)


Muda wa mkopo wa Dele Alli katika klabu ya Besiktas hautafanywa kuwa wa kudumu msimu wa joto, huku Everton wakitarajiwa kusitisha kandarasi ya kiungo huyo Mwingereza mwenye umri wa miaka 26. (Football Insider)


Thierry Henry amekataa nafasi ya kuwa kocha mkuu wa timu ya wanawake ya Ufaransa. (Le Figaro - kwa Kifaransa)


Klabu za Manchester United, Newcastle, Brighton na Brentford zimeonyesha nia ya kumnunua kiungo wa kati wa Uhispania na Celta Vigo Gabri Veiga pamoja na vilabu vingine vya Premier League pia hapo awali vilivyoonyesha nia ya kumtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. (90 Min)


Winga wa Brighton Solly March, 28, anatazamiwa kusaini mkataba mpya na klabu hiyo wakati mkataba wake wa sasa ukitarajiwa kumalizika msimu huu wa joto. (The Athletic)


Wolves wako tayari kumpa mkataba mpya nahodha na kiungo wa kati wa Ureno Ruben Neves, 26. (90 Min)


Bayer Leverkusen wana nia ya kumsajili beki wa West Ham na Jamhuri ya Czech Vladimir Coufal, 30. (Football Insider)


Crystal Palace watafanya uamuzi kuhusu mustakabali wa meneja Patrick Vieira wakati wa mapumziko ya kimataifa. (Telegraph - usajili unahitajika)


Beki wa zamani wa Tottenham na England Danny Rose, 32, anafanya mazoezi na klabu ya York City inayoshiriki Ligi ya Taifa, akiwa hana klabu tangu mkataba wake wa Watford ulipokatizwa mwezi Septemba. (Sun)


BBCDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz