Mshambuliaji wa Manchester City Erling Haaland amejiondoa kwenye kikosi cha Norway kwa ajili ya mechi yao ya kwanza ya kufuzu Euro 2024 kutokana na majeraha.
Haaland, 22, alipata tatizo la paja baada ya kufunga hat-trick katika ushindi wa 6-0 wa City dhidi ya Burnley kwenye robo fainali ya Kombe la FA Jumamosi.
Imeelezwa kuwa atakosa mechi za Norway dhidi ya Uhispania na Georgia katika Kundi A.
"Erling alichukua uamuazi huu alipogundua kwamba hangeweza kupigania timu," kocha wa Norway Stale Solbakken alisema.
"Kwa bahati nzuri, tuna vijana wapambanaji, wenye talanta na mshikamano kuhakikisha tunafanya vizuri katika mechi zinazofuata."
Daktari wa timu ya taifa ya Norway Ola Sand aliongeza: "Baada ya kufanya vipimo na uchunguzi jana ilibainika kuwa hatafanikiwa kuwahi mechi dhidi ya Uhispania na Georgia. Ni vyema akapata matibabu katika klabu yake"
No comments:
Post a Comment