Ujumbe mzito kutoka Kwa viongozi wa Simba baada ya Simba kutinga Robo Fainali ligi mabingwa - EDUSPORTSTZ

Latest

Ujumbe mzito kutoka Kwa viongozi wa Simba baada ya Simba kutinga Robo Fainali ligi mabingwa


Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA

Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA

Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba, Salum Abdallah 'Try Again' amesema kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ni moja ya malengo yao na kusisitiza wanaelekea kufikia hatua waliyokuwa wanaitamani miaka mingi yaani nusu fainali

Simba imetinga robo fainali kibabe baada ya kuifunga Horoya ya Guinea kwa mabao 7-0 ikifikisha pointi tisa ikiwa nyuma ya Raja Casablanca iliyokusanya pointi 13 ikiongoza Kundi C, Horoya ikiwa ya tatu na pointi nne na Vipers inaburuza mkia na pointi mbili kila timu ikicheza mechi tano.

Try Again amebainisha kuwa malengo ya klabu hiyo yalikuwa ni kuhakikisha wanaitengeneza Simba kuwa tishio ambayo inaweza kupambana na timu zingine kubwa zaidi Afrika sehemu ambayo ndio wanaelekea sasa

"Tulikuwa kwenye mtihani mkubwa wa kuhakikisha tunaiona Simba ikitinga hatua ya robo fainali hili limefanikiwa. Tulibezwa sana kwamba tuna kikosi kibovu, lakini safari inaendelea sasa na huko tuendako pia tuna nafasi ya kufanya vizuri pamoja na wengi kuzungumza mambo mengi"

"Tutawajibu kwa vitendo mpira unachezwa uwanjani na sio midomoni mwa watu kama ingekuwa hivyo kwa kuzungumzwa Simba inafungwa tusingeweza kufika hapa tulipo sasa tusubiri dakika nyingine tutakazozipata matokeo ndio yataamuliwa na tupo tayari kupambana na yeyote." alisema Try Again.

"Licha ya kupenya robo fainali, mikakati yatu ni kuifanya Simba kuwa kwenye ushindani na timu kama Raja Casablanca iliyotuonyesha ubora na tumejifunza kitu kutoka kwao na vile tuna mchezo dhidi yao kukamilisha ratiba tutaendelea kwenda kupambana na kujifunza ili kujipanga kwa robo fainali"

"Tunataka kuwa na timu bora na ya ushindani yenye kutamba Afrika na nje ya mipaka ya bara hili. Hapa tulipo ni mwanzo tena wa mbali sana katika kusuka klabu ambayo haitakuwa na mpinzani wa kushindana nayo," aliongeza Try Again.

Simba itasafiri Morocco kumalizia mechi ya makundi itakayopigwa Aprili 1 dhidi ya Raja Casablanca ambao waliwafunga mabao 3-0 nyumbani

Katika hatua ya robo fainali, Simba inaweza kukutana na Mamelodi, Esperance au Wydad Casablanca ambazo zinaonekana kuwa nafasi nzuri ya kumaliza vinara wa makundi yao

Mwanaspoti



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz