Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mshambulizi wa Paris Saint-Germain Mbappe, 24, amekubali jukumu hilo baada ya mazungumzo na kocha Didier Deschamps
Mchezo wake wa kwanza kama nahodha utakuwa wa Ijumaa wa kufuzu kwa Euro 2024 dhidi ya Uholanzi Uwanja wa Stade de France
Itakuwa mechi ya kwanza ya Les Bleus tangu kushindwa kwenye fainali ya Kombe la Dunia huko Doha mnamo Desemba 18.
Kipa wa Tottenham Lloris, 36, alimaliza soka lake la kimataifa mwezi Januari, wiki chache baada ya Argentina kuwashinda Wafaransa hao kwa mikwaju ya penalti kufuatia mechi ya kusisimua iliyoisha 3-3 katika muda wa ziada.
Lloris alikuwa nahodha kwa zaidi ya muongo mmoja. Mshambulizi wa Atletico Madrid Antoine Griezmann alitangazwa kuwa makamu wa nahodha baada ya beki wa kati wa Manchester United Raphael Varane pia kutundika daruga zake kufuatia kushindwa na Argentina mwezi Desemba.
Mbappe, ambaye alifunga hat-trick kwenye fainali ya Kombe la Dunia, alikuwa akihusishwa pakubwa na nafasi ya unahodha kwa wiki kadhaa
No comments:
Post a Comment