Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA
Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mshambuliaji hatari wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Fiston Mayele ambaye ameitwa kwenye kikosi cha timu ya DR Congo kinachojiandaa na michezo ya kufuzu AFCON 2023 dhidi ya Mauritania, amesema hatarudi tena Tanzania.
DR Congo inajiandaa na mchezo huo utakaopigwa keshokutwa Ijumaa (Machi 24) katika Uwanja wa Japoma mjini Douala nchini Cameroon, kasha timu hizo zitarudiana Machi 29 katika Uwanja wa Stade Cheikha Ould Boïdiya, mjini Nouakchott.
Mayele ambaye aliondoka jijini Dar es salaam juzi Jumatatu (Machi 20) baada ya kumaliza jukumu la kuivusha Young Africans kutoka hatua ya Makundi hadi Robo Fainali dhidi ya US Monastir, amesema tayari ameshazungumza na uongozi wa klabu na wamekubaliana atabaki DR Congo.
Amesema maamuzi hayo yamekuja kutokana na ratatiba ya mchezo ujao wa Kundi D, Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya TP Mazembe ambao watakuwa nyumbani mjini Lubumbashi mapema mwezi ujao.
“Tunakutana na TP Mazembe Aprili 2 na mimi nitakuwa na mchezo wa marudiano na Mouritania ugenini Machi 28, nitarudi nyumbani DR Congo na timu baada ya mchezo wetu wa pili na Mauritania. Hivyo nitaungana na wenzangu huku.”
“Suala la kwamba ni mchezo wa kukamilisha ratiba linabaki kwa mashabiki sisi kama wachezaji tunakwenda kupambana kuhakikisha tunapata matokeo ya ushindi ili kuendelea kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kuongoza kundi.” Amesema Mayele
Amesema anaiheshimu TP Mazembe na hawataingia kwenye mchezo huo kwa kujiamini kutokana na matokeo waliyoyapata katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, hivyo wenyeji wao watahitaji kulipa kisasi na kutunza heshima ya kushinda nyumbani kwao.
Young Africans inaongoza msimamo wa Kundi D, Kombe la Shirikisho Barani Afrika ikiwa na alama 10 sawa na US Monastir iliyozidiwa tofauti ya mabao ya kufungana kufungwa.
TP Mazembe inaburuza mkia wa Kundi hilo ikiwa na alama 03, ikitanguliwa na AS Real Bamako inayoshika nafasi ya tatu kwa kuwa na alama 05.
No comments:
Post a Comment