Conte awapa makavu wachezaji na Mabosi wa Tottenham baada ya kutoa share dhidi ya Southampton hapo jana - EDUSPORTSTZ

Latest

Conte awapa makavu wachezaji na Mabosi wa Tottenham baada ya kutoa share dhidi ya Southampton hapo jana

Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA

Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
 

Meneja wa Tottenham, Antonio Conte, aliwalaumu wachezaji wake baada ya kutangulia kwa mabao mawili na kulazimishwa sare ya 3-3 dhidi ya Southampton, akihoji vikali motisha yao na malengo ya klabu


Muitaliano huyo, anayetarajiwa kuondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu, pia alitia shaka mustakabali wake kwa kumkosoa mmiliki, Joe Lewis, na mwenyekiti wa klabu, Daniel Levy.


"Kwangu mimi hii haikubaliki," Conte alisema, James Ward-Prowse baada ya kufunga penalti kukamilisha kurejea kwa Saints katika sekunde za mwisho. Tunaongoza 3-1, lakini tunaruhusu kufungwa mabao mawili kirahisi"


Conte, akijibu maswali mawili tu katika dakika 10, alienda mbali zaidi kulaumu sare hiyo ambayo iliharibu matumaini ya Tottenham kumaliza kwenye top four


"Nadhani ni bora kuingia kwenye shida, sisi sio timu, Sisi ni wachezaji 11 wanaoingia uwanjani. Ninaona wachezaji wenye ubinafsi, wachezaji ambao hawataki kusaidiana na wasioweka moyo wao kwenye timu. Msimu huu ikilinganishwa na uliopita, tumefanya vibaya sana"


"Imekuwa hivi kwa miaka 20 sasa tunacheza tu kujifurahisha, haishangazi kuona timu haijashinda taji lolote katika kipindi hicho. Hakuna dhamira ya dhati ya kubadilisha hali hii," alisema Conte



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz