Yanga kuisaka robo fainali mbele ya US Monastir leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga kuisaka robo fainali mbele ya US Monastir leo

Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA

Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
 
Baada ya kuwashuhudia watani zao Simba wakitinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika kibabe kwa ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Horoya Ac, leo ni zamu ya Wananchi Yanga ambao wanashiriki michuano ya kombe la Shirikisho


Yanga itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili US Monastir katika mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali


Yanga wanahitaji ushindi ili kutinga robo fainali kuweka rekodi yao mpya katika michuano hiyo


Hii ni mara ya tatu kwa Yanga kucheza hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho lakini mara mbili ilishindwa kupenya robo fainali


Msimu huu Yanga imeonyesha ubora na kwa hakika Wananchi watajilaumu wenyewe kama watashindwa kutinga robo fainali


Wanahitaji kukata tiketi yao mapema ili kuondoa presha katika mchezo wa mwisho ambao watakuwa ugenini dhidi ya TP Mazembe


Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema kikosi chake kiko tayari akiwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa leo kuishangilia timu yao

Mechi itakuwa live kwenye app hii Bofya hapa kuidownload app ili uweze kuitazama mechi Mubashara kupitia simu Yako
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz