Alicho kisema Injinia Hersi baadae ya Yanga kutinga Robo Fainali

Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA

Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Rais wa klabu ya Yanga Injinia Hersi Said amewapongeza mashabiki na Wanachama kwa kuiunga mkono timu yao katika nyakati zote na sasa wamefanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika

Akizungumza baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya US Monastir jana, Hersi alisema kuwa haikuwa rahisi kwao kufikia mafanikio waliyopata lakini umoja na ushirikiano kutoka kwa kila Mwanayanga ni sehemu ya chachu ya mafanikio hayo

Hersi alisema mwanzoni waliweka malengo ya kucheza hatua ya makundi wakafanikiwa, kisha wakaweka malengo ya kutinga robo, wamefanikiwa sasa wanalenga kufika mbali zaidi katika michuano hiyo

"Nawashukuru sana Wanayanga kwa nguvu walioionesha kuiunga mkono timu yao mpaka tumepata haya matokeo, walikuwa nyuma ya timu katika matokeo mazuri na mabaya na sasa tumeingia Robo Fainali"

"Safari bado haijaisha, tulikuwa na malengo ya kuingia kwenye Makundi, tumevuka Makundi na kuingia Robo Fainali. Kama tulivyosema mwanzo safari bado haijaisha, twendeni tukaiunge timu mkono kwenye Robo Fainali, huwezi kujua inaweza kuwa Nusu Fainali, Fainali au Ubingwa," alisema Hersi

Yanga inaongoza kundi D ikiwa na alama 10 sawa na US Monastir lakini Yanga ina uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa kulinganisha na US Monastir

Yanga inahitaji kushinda mchezo wa mwisho dhidi ya TP Mazemba ambao utapigwa DR Congo April 02 ili kujihakikishia kumaliza kinara wa kundi

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post