Serikali yatia mkono stars kufuzu Afcon 2023 yatoa bonasi ya mil 500 endapo stars watafanya jambo hili - EDUSPORTSTZ

Latest

Serikali yatia mkono stars kufuzu Afcon 2023 yatoa bonasi ya mil 500 endapo stars watafanya jambo hili

Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA

Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Serikali itatoa kiasi cha Shilingi Milioni 500 endapo timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) itafuzu kushiriki Fainali za Kombe la Mataifa Barani Afrika Afcon 2023 michuano itakayofanyika mwakani 2024 nchini Ivory Coast.


Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Machi 20, 2023 jijini Dar es Salaam, Dkt Chana alisema Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Hamis Mwinjuma ataongoza hamasa kuelekea mchezo dhidi ya Uganda ambao utapigwa March 24 huko Misri na marudiano kupigwa jijini Dar es salaam, March 28.


"Nawaomba Watanzania tujitokeze kwa wingi kuishangilia Taifa Stars katika mchezo wa tarehe 24, Machi 2023 dhidi ya Uganda (The Cranes) ambao utakaochezwa katika mji wa Ismailia nchini Misri na mchezo wa marudiano utachezwa Machi 28, 2023 Uwanja wa Benjamini Mkapa" alisema Mhe. Chana.


Aidha, amewataka wadau wa mchezo huo ikiwemo Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na mashabiki kumuunga mkono Kocha wa Timu hiyo Bw. Adel Amrouche, huku akiwasistiza wachezaji wajitume ili waweze kufanya vizuri katika nashindano hayoDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz