YANGA yatoa tiketi 10,000 Bure kwa Mashabiki
CAF Confederation Cup 2022/2023, Makundi ya CAF Confederation Cup, Makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika 2022/2023, Yanga yatupwa Tunisia CAF Confederation Cup, Droo ya CAF Confederation Cup 2022/2023,, Droo ya Makundi CAF Confederation Cup 2022/2023, Droo ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika 2022/2023, Yanga vs Club Africain, Young Africans SC vs Club Africain,, UNICEF Tanzania, Young Africans, Yanga SC, Club Africain vs Yanga SC.
UONGOZI wa Klabu ya Yanga SC kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF) umezindua kampeni ya kuhamasisha na kutoa Elimu kwa wakazi wa Jiji la Dar Es Salaam kuhusu Chanjo ya UVIKO -19 na Virusi vya Ebola.
Kampeni hii ya siku 5 itaanza Jumamosi kwa gari Maalum la Matangazo kupita kwenye Mitaa Mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam kwaajili ya kuwafikia wananchi kwa karibu na kutoa Elimu na Chanjo ya UVIKO 19.
Mtendaji Mkuu wa Yanga SC, Andre Mtine amesema kuwa kwenye hizi siku 5 kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho la CAF dhidi ya Club Africain ya Tunisia, utakaochezwa November 02, 2022 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Klabu hiyo itatoa Zawadi Mbalimbali kwa Wananchi Watakaoshiriki kwenye zoezi hili la kupata Chanjo ya UVIKO-19.
“Tutagawa tiketi 10,000 za mzunguko kwaajili ya kushuhudia mchezo wa Kombe la Shirikisho kwa mashabiki wetu Watakaoshiriki Kampeni hii ya kupata Chanjo ya UVIKO 19. Pia tutakuwa na zawadi mbalimbali kama Kofia na Jezi za Yanga kwa Mashabiki.
WAFAHAMU Club Africain Wapinzani wa Yanga CAF Confederation Cup 2022/2023
“Mbali na zawadi hizo, pia mashabiki wetu watakaokuja kwenye vituo maalum vitakavyoandaliwa kwaajili ya kupata Chanjo watapata fursa ya kupiga picha na Makombe yetu matatu tiulioshinda msimu uliopita. Niwaombe Mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi katika maeneo tutakayopita ili kupata Elimu na chanjo ya UVIKO -19 na virusi vya Ebola,” amesema Mtine.
Naye Mkurugenzi wa Jackson Group, ambao ni wawakilishi wa Klabu ya Yanga kwenye upande wa Masoko, Kelvin Twissa alitaja maeneo tofauti ya Jiji la Dar Es Salaam ambayo Kampeni hii itapita kwa lengo la kutoa elimu ya virusi vya Ebola na chanjo ya UVIKO 19.
Jumamosi gari la Matangazo litapita kwenye Masoko ya Karume, Buguruni, Ilala, Magomeni na Mabibo. Siku ya pili, Jumapili, gari litaanza Ferry Kigamboni, Mjimwema, Kibada, Tandale Sokoni na kumalizia Manzese kwa Bakhresa.
Siku ya tatu, kampeni itaanza Ubungo maeneo ya Riverside na kuelekea Maeneo ya Kimara Temboni, Mbezi mwisho kituo cha mabasi kisha kukita Kambi kwenye kituo cha mabasi cha Magufuli na kumalizikia Kibamba CCM.
Jumanne, hamasa yetu ya kutoa Elimu na kupata chanjo ya UVIKO -19 na virusi vya Ebola itaanza kwenye soko la Mwananyamala na Kawe kisha tutaelekea Tegeta kwa ndevu, Boko Magengeni na kumalizia kituo cha mabasi cha Bunju.
Siku ya 5 gari itaanzia Buza kwa Mama Kibonge, Tandika Sokoni kisha kuja Mbagala Zakhem kisha mashabiki na Wanachama wa Yanga watakutana kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya kupata chanjo ya UVIKO -19 na kuingia Uwanjani kwajili ya kutazama Mchezo wa Kombe La Shirikisho la CAF dhidi ya Club Africain, utakaoanza saa 10:00 Jioni.
The post YANGA yatoa tiketi 10,000 Bure kwa Mashabiki appeared first on Nijuze Mpya.
No comments:
Post a Comment