SIMBA Queens yapokelewa vizuri Morocco
SHIRIKISHO la Soka nchini Morocco (FRMF) limeipatia Mapokezi mazuri timu ya Simba Queens tangu iwasili nchini Morocco jana kwaajili ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.
Hayo yamethibitishwa na Meneja wa Timu, Seleman Makanya na kuongeza kuwa Mapokezi hayo ni kuanzia timu ilipowasili Morocco ambapo waliipeleka timu hiyo hotelini ilipofikia huku taratibu zote stahiki zikifuatwa.
Makanya ameongeza kuwa pia Watanzania wanaoishi Jijini Casablanca nao wameipatia Mapokezi mazuri Simba Queens kiasi cha kujiona kama wapo nyumbani Tanzania.
“Tumesafiri na wachezaji 25, tumefika salama Morocco jana jioni tunamshukuru Mungu tumepata mapokezi mazuri, hakuna changamoto yoyote tuliyokutana nayo mpaka sasa. FRMF imetupokea vizuri,” amesema Makanya.
Baada ya kuwasili salama jana Wachezaji walipewa Mapumziko na leo usiku wataanza rasmi mazoezi kujiandaa na michuano huku wakiendelea kuzoea mazingira.
The post SIMBA Queens yapokelewa vizuri Morocco appeared first on Nijuze Mpya.
No comments:
Post a Comment