RATIBA ya Simba Queens Klabu Bingwa Afrika
SHIRIKISHO la Soka barani Afrika (CAF) limeweka wazi ratiba ya Ligi ya Mabingwa upande wa Wanawake ambayo itaanza October 30, 2022 nchini Morocco.
Timu ya Simba Queens ya Tanzania ambayo inawakilisha ukanda wa Afrika Mashariki na Kati itafungua dimba kwa dhidi ya wenyeji AS FAR kutoka Morocco mchezo utakaopigwa hiyo hiyo October 30, 2022.
Baada ya mchezo huo Simba Queens itapata siku mbili za kufanya mazoezi kabla ya kushuka dimbani kuikabili Determine Girls ya Libya, November 02, 2022.
Simba Queens itacheza tena mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi November 05, 2022 kwa kuikabili Green Buffalos ya Zambia.
Michuano hiyo inajumuisha timu nane zilizopangwa katika Makundi mawili ambapo kila kundi litatoa timu mbili zitakazofuzu hatua ya Nusu Fainali ya Michuano hiyo.
The post RATIBA ya Simba Queens Klabu Bingwa Afrika appeared first on Nijuze Mpya.
No comments:
Post a Comment