KOCHA Simba afunguka kuelekea Mchezo vs Yanga October 23 2022
Yanga vs Simba October 23 2022, Simba SC vs Yanga SC, Yanga vs Simba 23 October 2022, Simba Sports Club vs Young Africans SC 23 October 2022, Simba SC vs Yanga SC NBC Premier League, Yanga vs Simba Yanga Ligi Kuu, Yanga vs Simba watani wa Jadi, Matokeo Simba vs Yanga October 23 2022, Kariakoo Derby, Dar es Salaam Debry 23 October 2022, Derby ya Dar es Salaam Simba SC vs Yanga SC, Yanga vs Simba October 23 2022, Simba Sports Club vs Young Africans SC October 23 2022, Yanga SC vs Simba SC 23 October 2022.
KOCHA Mkuu wa Klabu ya Simba SC Juma Mgunda, ameweka wazi kuwa mchezo wa Derby ya Dar es Salaam au Kariakoo dhidi ya watani wao Yanga SC, hautabiriki na utakuwa mgumu.
Mgunda amesema kuwa mchezo wa watani wa Jadi siku zote ni mgumu ndiyo maana anaendelea kukiandaa kikosi ambapo Wachezaji wanajitahidi kufuata maelekezo yake mazoezini.
Ingawa itakuwa ni mchezo wake wa kwanza wa Derby, Mgunda amesema hana presha ya mechi ingawa anahafamu itakuwa ngumu na ya kuvutia kutokana na ubora wa timu zote mbili kwa sasa.
“Mchezo utakuwa mgumu, siku zote mechi ya Derby haijawahi kuwa rahisi nasi tunajua, tunaendelea na mazoezi, nafurahi jinsi wachezaji wangu wanavyopokea maelekezo mazoezini.
“Ni kweli utakuwa mchezo wangu wa kwanza wa Derby lakini sina presha, najua itakuwa mechi nzuri kikubwa tuwaombee wachezaji waamke salama siku hiyo,” amesema Mgunda.
Mchezo huo utapigwa Jumapili hii ya October 23, 2022 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kuanzia majira ya saa 11:00 Jioni.
The post KOCHA Simba afunguka kuelekea Mchezo vs Yanga October 23 2022 appeared first on Nijuze Mpya.
No comments:
Post a Comment