KOCHA Mkuu Taifa Stars apigwa chini - EDUSPORTSTZ

Latest

KOCHA Mkuu Taifa Stars apigwa chini

KOCHA Mkuu Taifa Stars apigwa chini

KOCHA Mkuu Taifa Stars apigwa chini

KOCHA Mkuu Taifa Stars apigwa chiniSHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetangaza kuwa limefikia makubaliano ya kumuondoa kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Kim Poulsen kwenye benchi la ufundi pamoja na wasaidizi wake.

Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Ndimbo, imeeleza kuwa pande zote mbili zimefikia makubaliano hayo baada ya kikao cha pamoja.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa Poulsen ataendelea kubaki katika timu za taifa za vijana mpaka mkataba wake utakapokamilika na kwamba kwa sasa benchi la ufundi la Taifa Stars litakuwa chini ya kocha Hanour Janza akisaidiwa na Meck Maxime huku Juma Kaseja akiteuliwa kuwa kocha wa magolikipa.

KOCHA Mkuu Taifa Stars apigwa chiniAidha Tanzania imejiweka njia panda kufuzu Michuani ya Wachezaji wa ndani (CHAN) mashindano yatakayofanyika nchini Algeria 2023 baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa bao 1-0 kutoka Uganda mchezo uliopigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam August 28,2022.

Akitokea benchi Mshambuliaji Travis Mutyaba aliwanyamazisha Watanzania waliohudhuria mechi hiyo baada ya kuipatia Tanzania bao la ushindi kwenye dakika ya 87.

Tanzania sasa ina mlima wa kwenda kupindua meza kwenye mchezo wa marudiano September 03,2022, Mchezo unatarajiwa kufanya kwenye uwanja wa St.Mary nchini Uganda.

The post KOCHA Mkuu Taifa Stars apigwa chini appeared first on Nijuze Mpya -| Pata Habari zote za Michezo kitaifa na Kimataifa, Tetesi na Usajili, Magazeti ya Michezo, Ratiba na Matokeo, Mahusiano Pamoja na Nafasi za Kazi.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz