VIGOGO, Simba SC wamekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Kimataifa wa Zambia, Moses Phiri kutoka Zanaco ya kwao.
Mchezaji huyo ambaye kwao anaitwa ‘Moses of our time’ amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Wekundu wa Msimbazi na anakwenda kucheza pamoja na Wazambia wenzake wawili, viungo Rally Bwalya na Clatous Chota Chama.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Buildcon msimu uliopita akiwa na Zanaco amefunga mabao 14 kwenye Ligi Kuu ya Zambia akishika nafasi ya pili nyuma ya mfungaji Bora wa msimu, Ricky Banda aliyemaliza na mabao 16.
Phiri alikuwa Mfungaji Bora wa Ligi ya Zambia msimu wa 2020/21 alipomaliza na mabao 17 na kuiwezesha Zanaco kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika.
No comments:
Post a Comment