PONGEZI nyingi zimemiminika Yanga SC kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jana kufuatia ushindi wa 3-0 dhidi ya Coastal Union jana Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga yalifungwa na washambuliaji wake Wakongo, Fiston Kalala Mayele, mawili dakika ya 35 na 68 na Chico Ushindi Wakubanza dakika ya 52.
Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 67 katika mchezo wa 27, ambazo hakuna inayoweza kufikisha, kwani mabingwa wa misimu minne iliyopita wenye pointi 51 sasa wanaweza kufikisha pointi 66 kama watashinda mechi zao zote tano zilizosalia.
Hilo kina kuwa taji la 28 na la rekodi la Ligi Kuu kwa Yanga,ambao waliuanza msimu kwa ushindi wa Ngao ya Jamii wakiwafunga 1-0 watani, Simba Uwanja wa Mkapa.
Julai 2 watamenyana na Coastal Union katika Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kuwania taji la tatu la msimu.
No comments:
Post a Comment