Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa Ashitakiwa kwa Kosa la Jinai - EDUSPORTSTZ

Latest

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa Ashitakiwa kwa Kosa la Jinai



MKUU wa Usalama wa zamani wa Afrika Kusini Arthur Fraser amemfungulia mashitaka ya kosa la jinai Rais wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa kwa tuhuma za utekaji na utoaji rushwa ili kuficha tukio la uhalifu lililotokea katika moja ya milki zake eneo la Limpopo ambako inakadiriwa wahalifu hao waliiba zaidi ya dola milioni 4 ambazo zilikuwa ni mali za Ramaphosa.

Mku huyo wa intelijensia na Usalama amefikisha shauri lake katika kituo cha Polisi cha Rosebank kilichopo Afrika Kusini.

Fraser amethibitisha kuwa wahalifu walikamatwa, wakahojiwa lakini cha kushangazwa walipewa rushwa ili walizime lile tukio la kuiba kiasi hicho cha pesa.


Cyril Ramaphosa Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini
Ofisi ya Rais imethibitisha kuwa Rais Ramaphosa ameshapata taarifa na atajibu tuhuma hizo muda si mrefu.


 
“Nimechukua maamuzi haya muhimu kufungua kesi dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa.” Alisema Fraser.


Rais Ramaphosa amesema atajibu tuhuma za jinai dhidi yake ndani ya muda mfupi ujao
Fraser amesema aliwapatia Polisi ushahidi na nyaraka zote muhimu ikiwemo Picha, Video, Akaunti za Benki pamoja na Majina ya watuhumiwa wote.

Amesisitiza kuwa vitendo vya Rais vilikuwa ni uvunjifu wa wazi wa sheria kwa kukumbatia uhalifu uliokuwa umepangwa.

Tayari Polisi wamethibitisha kwa vyombo vya habari kuwa kesi ya jinai imeshafunguliwa kwa Rais Ramaphosa na taratibu za kisheria zinaanza kutekelezwa mara moja.

Baada ya kumaliza utumishi wake Serikalini kama Mkuu wa Intelijensia na Usalama wa nchi ya Afrika Kusini, Arthur Fraser alipewa majukumu ya kuwa Msimamizi wa Uratibu wa Haki za wafungwa Magerezani.

Inakumbukwa mwaka jana yeye ndiye aliyeidhinisha Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma aondolewe gerezani kutokana na matatizo ya kiafya lakini baadaye ilikuja kugundulika kuwa sababu za Fraser hazikuwa na uzito na hatimaye Zuma akarudishwa tena gerezani kuendelea kutumikia hukumu yake ya kifunga cha miaka 15 kutokana na kosa la ukiukwaji wa Katiba ya nchi.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz