BEKI wa Kulia wa Tottenham Hotspurs raia wa Brazil Emerson Royal (23) amenusurika kuuawa kwa risasi baada ya kuvamiwa na wezi katika ukumbi wa starehe uliopo Jiji la Americana Kaskazini mwa Sao Paulo ambapo alikuwa anapiga picha na moja ya Maofisa wa Polisi waliokuwa nje ya eneo hilo.
Akielezea tukio hilo Royal anadai kuwa wezi hao walimlenga yeye na bunduki wakimlazimisha awapatie mali alizokuwa nazo lakini ndani ya dakika chache alitokea Askari Polisi akaanza kujibizana kwa kupigana risasi na wezi hao ambao baada ya majibizano ya risasi takribani 29 mwizi mmoja alijeruhiwa sehemu ya mgongo na hatimaye kutiwa nguvuni na Polisi.
Taarifa ya Polisi inadai mwizi huyo anaendelea vizuri baada ya kupelekwa hospitali na kupatiwa matibabu, na Emerson Royal ni mzima na hakupata jeraha lolote.
“Nitakushukuru daima” aliandika Royal kwenye ukurasa wake wa Instagram.
“Mungu hutuma Malaika wake duniani, nah ii imekuwa ikithibitika kila siku maishani mwangu, binadamu huyu mi namuita malaika, alihatarisha maisha yake kuokoa maisha yangu.” Aliongeza beki huyo wa kulia wa Brazil.
Royal aliyefanikiwa kucheza jumla ya michezo 41 ndani ya klabu ya Tottenham Hotspurs msimu uliopita yupo nyumabni kwao nchini Brazil kwa ajili ya mapumziko ya mwisho wa msimu na amekuwa akila bata na familia yake pamoja na rafiki zake katika ukumbi mpya wa starehe wa Trips.
The post Mchezaji wa Tottenham Hotspurs Anusurika Kuuawa Kwa Risasi appeared first on Global Publishers.
No comments:
Post a Comment