Shevchenko Aililia Familia Yake Ukraine - EDUSPORTSTZ

Latest

Shevchenko Aililia Familia Yake UkraineSTRAIKA mstaafu Andriy Shevchenko, amelia mbele ya kamera akiikumbuka familia yake inayopitia mateso ya vita nyumbani kwao Ukraine.

Shevchenko, 45, anakumbukwa zaidi akitamba AC Milan na hivi karibuni alifundisha Genoa inayoshiriki Serie A kwa miezi miwili tu kufuatia kuiongoza timu ya taifa ya Ukraine kwa miaka mitano.

Akizungumza na kituo kimoja cha televisheni nchini Italia, Shevchenko alieleza kukoseshwa raha kila anapoikumbuka familia yake iliyoamua kubaki Ukraine licha ya uvamizi unaoendelea chini ya majeshi ya Rais wa Urusi, Vladimir Putin. Alishindwa kujizuia na kujikuta akilia hadharani.

“Mama yangu, dada yangu na ndugu zangu wengine bado wapo Ukraine, naongea nao kila siku. Ulikuwa ni uamuzi wao kubaki,” alisema Shavchenko.


 
“Siwezi kuangalia kile kinachotokea katika nchi yangu bila kulia, Huwa wananiambia ukweli wa kinachoendelea Ukraine, majiji yanalipuliwa, watoto na wazee wanauawa. Tunahitaji kujaribu kuishawishi Urusi iache vita, itafute suluhisho la kidiplomasia.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz