Mpiga Picha wa Diamond Amuomba RADHI Mkewe kwa Kucheza Mziki na Gig Money - EDUSPORTSTZ

Latest

Mpiga Picha wa Diamond Amuomba RADHI Mkewe kwa Kucheza Mziki na Gig Money

Mpiga picha wa staa wa bongo fleva Diamond Platnumz kwa jina Lukamba baada ya shinikizo na michambo kutoka kwa wanamitandao hatimaye amemuomba mkewe radhi kwa kuonekana akicheza densi kwa njia ya kimahaba na mwanamitindo Gig Money kwenye Yatch wakati wa kusherehekea EP ya Diamond Platnumz ya FOA.

Lukamba alijipata kwenye upande hasi wa majasusi wa mitandaoni baada yao kumlimbikizia maneno ya soni kwamba anamdhalilisha mkewe kwa kucheza densi kimahaba na Gig Money lakini Lukamba aliandika kwenye Instagram yake ujumbe wa kutaka radhi kwa mkewe.


“Mke wangu nakiri nimekukosea, mara nyingine unapokuwa kwenye mazingira fulani unajisahau na kwenda na Vibe iliyopo, Nimejifunza, Nakubali Nilichokifanya ni upumbavu na siko proud nao, na hakuna mwanamke yeyote angependezwa kuona mwanaume wake tena MUME WA NDOA anafanya nilichokifanya, NISAMEHE MKE WANGU, ule sio ujana ni ujinga nimefanya na naomba radhi kwako, Nakupenda sana mke wangu na siko tayari kukupoteza, Nisamehe Mama,” aliandika Lukamba.

Alikiri makosa yake ila akajitetea kwamba alijisahau kwa furaha ya sherehe hizo kwenye Yatch na akajipata anakwenda na mrindimo uliokuwepo ila baadae alipojirudi ndio akagundua kwamba kitendo kile si kizuri kwa mkewe.

Mashabiki wengi wamempongeza mpiga picha huyo kwa hatua hiyo ambayo wengi waliitaja kuwa ya kijasiri kwani si rahisi kumpata mwanaume akijutia vitendo vyake na kuomba msamaha.

Je, unahisi kucheza densi na mtu ambaye hamna mahusiano naye ni moja ya njia za kuchepuka na unapaswa kuomba mpenzi wako msamaha?
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz