Matajiri Urusi wahamisha fesha Dubai - EDUSPORTSTZ

Latest

Matajiri Urusi wahamisha fesha DubaiMatajiri wa Urusi wameanza kuhamisha fedha zao kutoka Ulaya kwenda Dubai ili kukwepa vikwazo vya Magharibi vinavyoendelea kuwekwa kufuatia operesheni ya kijeshi ya Urusi nchini Ukraine, Mtandao wa Reuters umeripoti ukinukuu taasisi za kifedha na vituo vya sheria.

Dubai ambayo imekuwa kivutio cha watalii ulimwenguni, pia inachukuliwa kuwa kitovu cha biashara cha eneo la Ghuba. Taarifa zinasema kukataa kwa Umoja wa Falme za Kiarabu hivi karibuni kulaani operesheni ya kijeshi ya Urusi nchini Ukraine katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa inaonekana kutafsiriwa na matajiri wa Urusi kama mwaliko.

Kulingana na vyanzo vya Reuters, raia wa Urusi wamekuwa wakihamisha fedha zao kutoka Uswizi na Uingereza hadi Dubai, baada ya mataifa hayo mawili kuiwekea vikwazo Urusi na kutishia kufungia mali ya wafanyabiashara na wanasiasa mashuhuri wa Urusi.

Mwanasheria ambaye jina lake halikutajwa anayeishi Dubai aliambia reuters kwamba kampuni yake imepokea maombi kadhaa kutoka kwa mashirika ya Urusi kuhusu kuhamisha “fedha” kwenda Dubai.

Chanzo kingine, kilisema wateja wa Urusi walio na akaunti katika benki za kibinafsi mahali pengine walikuwa wakifungua akaunti na tawi la benki hiyo la UAE au na benki za ndani. Walibainisha kuwa idadi ya wateja wa Urusi ilikuwa imeongezeka.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz