Baba yake Tajiri wa GSM amefariki - EDUSPORTSTZ

Latest

Baba yake Tajiri wa GSM amefarikiMzee Said Mohamed ambaye ni Baba Mzazi wa Mfanyabiashara Ghalib Said Mohamed (GSM) amefariki dunia alfajiri ya leo March 1 2022 na anatazikwa leo saa kumi jioni kwenye makaburi ya kisutu Dar es salaam.

Marehemu Mzee Said ni Mfanyabiashara wa muda mrefu Tanzania ambapo alianzisha biashara ya kwanza mwaka 1955 kwa kuuza bidhaa ndogondogo Tanga lakini baadae alihamia kuuza nguo na kuhama kutoka Tanga hadi Songea ambako alijitanua katika kilimo cha korosho ambacho Familia yake imekiendeleza hadi leo.

Marehemu Mzee Said alistaafu mwaka 1996 na kuruhusu kizazi kilichofuatia kuchukua usukani wa kila siku wa biashara na kuamua kuhamia Dar es Salaam na kuwa Wasambazaji wakubwa wa mazulia ya PVC ndani ya Tanzania na nchi jirani.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz