Kwanini Ali Kiba Kamzidi Diamond Platnumz Katika Mapato ya Mirabaha - EDUSPORTSTZ

Latest

Kwanini Ali Kiba Kamzidi Diamond Platnumz Katika Mapato ya Mirabaha


Daah! ila wazee wa mirabaha noma kweli, yaani Diamond Platnumz ni mtu wa kupewa buku ten kweli😢😢😢.

Natania bana ila kimsingi ni kwamba tangu Alikiba amechukua zaidi ya Million saba kutokana na Mirahaba, watu wengi wameonekana wakilizungumzia hili na wanadis kwanini Alikiba amzidi Diamond.

Kwa maoni yangu binafsi, Kiukweli Alikiba amestahili pesa hizo, Maana ngoma zake zinachezwa MEDIA ZOTE TANZANIA.

PILI, Alikiba ametoa Album mwaka huu, hivyo mzunguko wa pesa ni mkubwa, ila kubwa zaidi ni hilo la ngoma zake kupigwa media zote.

Diamond hajapata mkwanja mrefu kwasababu nyimbo zake zinachezwa media chache sana, media kubwa zote mbali na wasafi media hazichezi ngoma zake, hivyo hawezi pata mkwanja wa maana. Pili mwaka jana kaachia ngoma chache sana, so hata zikipigwa hazitaleta positive impact kubwa.

Serikali inaanzisha hivi vitu katika wakati ngumu mno, maana kipindi hiki kuna matatizo makubwa sana katika sanaa, Media na wadau mbali mbali wa sanaa.

Siku hizi ni mwendo wa Uteam tu, hivyo kuna wasanii watakosa stahiki zao kwasababu tu ya Mabifu ya Hovyo kati ya Diamond na Media, Imagine wasanii wa WCB ngoma zao hazipigwi CLOUDS, EFM&TVE, EATV(sina uhakika kama bado wamewakazia) JE UNATEGEMEA WATAPATA PESA YA MAANA KWELI KWENYE MIRABAHA AU NDIO HIVYO WATAISHIA KUPATA BUKU JERO.

Hopetyga
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

2 comments:

  1. Thanks for your kind information. check our guide of best fishing rod

    ReplyDelete
  2. Thanks for sharing. visit our website bitjobz and check all latest jobs

    ReplyDelete

Edusportstz