Fayvanny "Kama Wameachana Kanye West na Kim Mimi na Rayvanny ni Nani Tusiachane" - EDUSPORTSTZ

Latest

Fayvanny "Kama Wameachana Kanye West na Kim Mimi na Rayvanny ni Nani Tusiachane"


BABY mama wa staa wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa almaarufu Rayvanny ambaye ni Fahyma, anasema kuwa, kama wameachana rapa wa Marekani, Kanye West na mwanamitindo Kim Kardashian, wao ni kina nani wasiachane?

Fayhma alikuwa akijibu maswali ya mashabiki wake kwenye Instagram baada ya kumposti bibi yake na kumsifia juu ya uzuri wake kwa kusema; “I miss you bibi (grandmother) yangu mzurimzuri, nyie halafu Wasambaa wazuri asikwambie mtu…”

Hapo ndipo mmoja wa mashabiki alipomuuliza; “Kama ninyi ni wazuri mbona uliachwa (na Rayvanny)

Baada ya kuulizwa hivyo ndipo Fahyma akamjibu; “Wameachana Kanye na Kim itakuwa mimi?”

Rayvanny na Fahyma waliachana mwaka juzi baada ya jamaa huyo kutangaza kuwa kwenye mapenzi mubashara na Paula Kajala; yule mtoto wa mwigizaji Kajala Masanja na prodyuza P Funk Majani.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

2 comments:

Edusportstz