Hatimae filamu ya Binti yaanza kuonekana kwenye platform ya NETFLIX - EDUSPORTSTZ

Latest

Hatimae filamu ya Binti yaanza kuonekana kwenye platform ya NETFLIXFilamu ya Binti iliyoandaliwa na director Seko Shamte kupitia Black Unicorn Studios, tayari imeanza kuruka leo 7 mwezi wa kwanza 2022 kupitia platform hiyo.

Seko Shamte amesema ina kibali cha kuonekana ulimwengu kote (Global acquisition) na siyo Africa tu, kwa hiyo watu wote wenye netflix duniani watapata fursa ya kuingalia.

Binti ilishinda tuzo yafilamu bora mwaka 2021 kwenye ZIFF na inaonekana Netflix wameona ina kiwango bora inayostahili kuonekana kwenye platform yao. Itakuwa ndiyo filamu ya kwanza iliyonadaliwa hapa hapa nyumbani, yenye waigizaji wa hapa nyumbani kuwepo kwenye Platforrm hiyo yenye subscribers millioni 209, duniani kote.

“Kiukweli ni jambo la kumshukuru na ningependa kuwajuza mashabiki ama wafuatiliaji wa filamu ya Binti kuwa imeanza itaanza kuonekana leo 7 January 2022 kupitia Platform ya NETFLIX”- Seko Shamte
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz