Atumia Mabango ya Matangazo Barabarani Kutafuta Mke - EDUSPORTSTZ

Latest

Atumia Mabango ya Matangazo Barabarani Kutafuta MkeMwanaume moja huko London aliyejulikana kwa jina la Muhammad Malik ameshangaza wengi jijini humo baada ya kutumia mabango ya matangazo makubwa kutafuta mke.

Muhammad amefikia hatua hiyo baada ya njia nyingine za kutafuta mke kufeli, mwanaume huyo mwenye miaka 29 ameweka mabango hayo London na Birmingham yakiwa na ujumbe: “Niokoe kutoka kwenye ndoa iliopangwa.”


Muhammad aliambatanisha na e-mail yake na baada ya kuweka tangazo hilo amesema tayari ameanza kupokea jumbe mbalimbali kutoka kwa wanawake wakitaka kuwa mke wake.

Muhammad ameongeza kwa kusema kuwa angetamani mtarajiwa wake ashiriki naye dini ya kiislamu na awe radhi kufata matakwa ya familia yake.

Mabango hayo ya matangazo yamepangwa kubaki mpaka Januari 14, mwaka huu.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz