Nyakati za Mwisho...Ashikiliwa kwa kumbaka mama mzazi - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Nyakati za Mwisho...Ashikiliwa kwa kumbaka mama mzaziJESHI la Polisi mkoani Dodoma linamshikilia mwanaume wa miaka 30 kwa tuhuma za kumbaka Mama yake mzazi mwenye umri wa miaka 75 tukio lililotokea Wilayani Kondoa mkoani hapa.

Pia mzee mwenye miaka 61 anashikiliwa na Jeshi hilo kwa tuhuma za kumbaka mjukuu wake mwenye umri wa miaka 11 ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne. Tukio lililotokea Wilaya ya Kongwa.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari jana Kamanda wa Polisi Dodoma, Onesmo Lyanga alisema Jeshi hilo limemkamata mwanaume (30) kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wake wa kiume katiika mtaa wa Mulua wilaya ya Kondoa.

Jeshi hilo pia linamshikilia mwanamke (24) mkazi wa Tampoli wilaya ya Kondoa kwa kumchoma na kitu cha ncha kali tumboni mume wake baada ya kumkuta amesimama na mwanamke mwingine.Majeruhi amelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Kondoa.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz