Mbunge Msukuma Ambae Ana Elimu ya Darasa la Saba Atunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima (PHD) - EDUSPORTSTZ

Latest

Mbunge Msukuma Ambae Ana Elimu ya Darasa la Saba Atunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima (PHD)
Mbunge wa Geita vijijini Joseph Kasheku Msukuma ametunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima PHD ya Siasa na Uongozi kutoka chuo cha The American Univercity USA cha nchini Marekani.

Msukuma na wenzake 15 akiwemo mwanaharakati Frola Lauo wa Nitetee Foundation aliyetunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima wa Falsafa mwingine ni aliyewahikuwa Waziri wa Kilimo ambaye ni Mbunge wa Vwawa Songwe Japhet Hasunga.

Shahada hizo wametunukiwa mkoani Dodoma na Profesa Madhu Krishan mwakirlshi wa chuo hicho.

Msukuma mwenye elimu ya darasa la saba amesema chuo hicho kimemfuatilia kwa kipindi cha miaka mitatu katika michango yake bungeni kupitia video za YOUTUBE na alikuwa akipigiwa simu mara kwa mara kwaajili ya kumfuatilia mpaka Desemba 5,2021 ambapo ametunukiwa heshima hiyo
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz