Kijana Mbaroni kwa Kumkata Kichwa Dada’ke Mjamzito na Kisha Kupiga Selfie na Kichwa - EDUSPORTSTZ

Latest

Kijana Mbaroni kwa Kumkata Kichwa Dada’ke Mjamzito na Kisha Kupiga Selfie na KichwaPolisi katika jimbo la Maharashtra – Magharibi mwa India wamemkamata kijana anayeshukiwa kumkata kichwa dadake mkubwa aliyekuwa mjamzito. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mwanamke huyo (19), alikuwa ameolewa na mwanamume bila idhini ya familia yake, maofisa wa polisi wa eneo hilo walisema.

Alikuwa akiwatengenezea kaka na mama yake chai aliposhambuliwa kwa mundu. Kijana huyo na mama yake kisha walijisalimisha kwa polisi.

Polisi wanashuku kuwa pia walipiga picha ya selfie na kichwa cha mwanamke huyo.


Ndugu huyo alipelekwa rumande kwa watoto baada ya wakili wake kusema kwamba alikuwa na umri wa chini ya miaka 18.

Hata hivyo, Ofisa mmoja wa polisi alisema wangepinga dai hili kortini kwa vile wamepata cheti kinachoonyesha kuwa ni mtu mzima. Mama yao aliwekwa chini ya ulinzi wa polisi.

Kisa hicho kilitokea katika wilaya ya Aurangabad, BBC Marathi iliripoti.

Mwathiriwa alitoroka Juni na kuolewa na mpenzi wake baada ya familia yake kupinga uhusiano wao.

Ingawa wote wawili walikuwa wa tabaka moja, familia yake haikumkubali kwa vile familia yake ilikuwa maskini kuliko yao.

Mwanamke huyo hakuwasiliana na familia yake sana baada ya ndoa yake lakini mama yake alimtembelea wiki moja kabla ya mauaji. Polisi walisema alijua kwamba binti yake alikuwa mjamzito.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz