Hichi Ndio Kifaa Kinachosaidia Binadamu Kujiua Kwa Urahisi..Yaani Unakufa Fasta Bila Kusikia Maumivu - EDUSPORTSTZ

Latest

Hichi Ndio Kifaa Kinachosaidia Binadamu Kujiua Kwa Urahisi..Yaani Unakufa Fasta Bila Kusikia MaumivuUswizi imeripotiwa kuidhinisha matumizi ya hiki kifaa cha kujimalizia (kijiua) kiitwacho” Sarco capsule”. 2022

Yaani unaambiwa hiki kifaa unaaga dunia ndani ya sekunde 30 tu, kiko veery comfortable na unakufa kwa amani kabisa bila kukuruka wala nini yaani kama umelala tu🙄🙄, maelezo ya Dr Nitschke

Kwanza ukiingia humo kuna maswali kadhaa (recorded) utayajibu halafu wewe ndie unae bonyeza kitufe kwa ndani ili kujiua, na unaweza kuipeleka eneo lolote la kujiulia, kama ni nje au ndani, (naona hata beach ukitaka fresh tu)


Ukibonyeza kitufe mle mdani, Nitrojeni inajaa ndani na kusababisha oksijen kuwa chini kutoka asilimia 21 hadi asilimia 1 ndani ya sekunde 30 tu na kupoteza fahamu.

Kifo hutokea kutokana na hypoxia (oksijeni kuwa chini katika tishu za mwili) na hypocapnia (kupunguzwa kwa kabon daioksaid katika damu).

"Faida kwa mtu anayeitumia ni kwamba hawahitaji kupata ruhusa yoyote, hawahitaji daktari maalum kujaribu kuingiza sindano, na hawahitaji kupata dawa ngumu," alisema Dr. Nitschke ambae ndie mgunduzi wa Sarco Capsule alipokuwa akifanya demostration mwakajana.Sarco imetengenezwa na shirika lisilo la faida la kimataifa la “Exit International” lenye makao yake makuu Australia.

Takriban watu 1,300 walikufa kwa kusaidiwa kujiua nchini Uswizi mnamo 2020 kwa kutumia huduma za mashirika makubwa zaidi ya kusaidia kujiua nchini humo, Exit na Dignitas, kulingana na ripoti ya SwissInfo.

Hivi sasa, kujiua kwa kusaidiwa nchini Uswizi kunamaanisha kumeza capsule iliyojazwa controlled substances ambayo humfanya mtu awe katika coma (hali ya kukosa fahamu) kabla hajafa.

Watu husaidiwa kujiwa kama familia zao zikikubaliana eidha kutokana namateso ya maumivu makali ya magonjwa kama kansa na yale yasiotibika au mtu mzima sana ambae anaona bora ajifie zake maana haoni sababu ya kuendelea kuishi na sababu zingine 🤷🏾‍♀️
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz