Kagere, Wawa, Banda wavunjiwa mikataba Simba - EDUSPORTSTZ

Latest

Kagere, Wawa, Banda wavunjiwa mikataba SimbaKLABU ya soka ya Simba imevunja mikataba ya nyota wake wanne wa kigeni wakiwemo mastaa wao aliokuwa tegemeo katika kikosi hicho kwa misimu kadhaa, beki wake Raia wa Ivory Coast, Pascal Wawa na mshambuliaji wake, Mnyarwanda, Meddie Kagere. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). 

Mbali na mastaa hao wawili tegemeo, nyota wengine wa kimataifa waliotemwa ni Peter Banda aliyesajiliwa kwenye dirisha kubwa la usajili mwezi Agosti na kiungo mshambuliaji Dancan Nyoni Raia wa Malawi ambaye ameshindwa kuonesha makali yake toka asajiliwe klabuni hapo.

Simba imeamua kuvunja mkataba na wachezaji hao, ili kupata nafasi ya kusajili wachezaji wengine wa kigeni kwenye dirisha dogo la usajili.


Pascal Wawa
Ikumbukwe hivi karibuni klabu hiyo ilivunja mkataba kwa makubaliano maalumu na kocha wake msaidizi Thiery Hitimana raia wa Burundi.


 
Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wameamua kufanya maboresho kwenye kikosi chao kufuatia kusuasua hivi karibu.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz