Makala Agness: Nililipwa Mil 11 Kwenda Kufanya Mapenzi Nigeria - EDUSPORTSTZ

Latest

Makala Agness: Nililipwa Mil 11 Kwenda Kufanya Mapenzi NigeriaKAMA ni mfuatiliaji wa mambo yanayoendelea mitandaoni, basi jina la Aggy Baby siyo geni kwako. Akifahamika zaidi kwa jina la Agness wa Mahari Milioni 500, alikuwa gumzo mitandaoni baada ya kutangaza kwamba mwanaume anayetaka kumuoa anapaswa kulipa mahari ya shilingi milioni 500.

Kama hiyo haitoshi, akazua tena gumzo kwa kumpa ofa mchezaji wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ya kumuoa bure kutokana na kukoshwa na uwezo wake uwanjani.

Mbali na drama za hapa na pale, Aggy Baby ambaye jina lake halisi ni Agness Suleiman amejitwalia umaarufu kupitia Tamthiliya za Panguso na Huba zinazorushwa DSTV.

Kubwa kabisa ni msanii mkali wa Bongo Fleva akiwa amesikika kwenye ngoma kadhaa zikiwemo Wanipa na Watajuaje zinazokiwasha kwenye miandao mbalimbali;


 
Gazeti la IJUMAA limepiga stori na Aggy Baby ambapo amefunguka mambo mbalimbali kuhusu maisha yake;

IJUMAA: Tukio gani kubwa ambalo hutalisahau maishani mwako?

AGGY BABY: Nakumbuka, nilitumiwa Dola za Kimarekani 5000 ambazo ni sawa na shilingi milioni 11 na mwanaume mmoja ili niende Nigeria nikashiriki naye mapenzi. Sitosahau!

IJUMAA: Ilikuwaje?

AGGY BABY: Tulikutana mtandaoni, akaanza kunitumia ujumbe (DM) Instagram na kunieleza alivyotokea kunipenda, aliniambia anaweza akanifanya niinjoi na atanipa kila kitu nitakachohitaji.

IJUMAA: Enhe! Ikawaje?

AGGY BABY: Alitaka kuniaminisha kuwa anaweza kunigharamia kwa kiasi chochote cha pesa, akanitumia Dola 5,000 na kuniambia nianze kujiandaa atanitumia tiketi ya ndege ili niende Nigeria tukakutane. Sikuzikataa, nikazipokea, lakini sikwenda.

IJUMAA: Kwa nini hukwenda?

AGGY BABY: Sikuona haja ya kupoteza utu wangu kwa shilingi milioni 11, lakini kubwa zaidi, yule Mnigeria alinionesha dalili za kutokuwa mwaminifu tangu mwanzo kabisa kwa sababu alikuwa pia anamtaka rafiki yangu kimapenzi, nikashtuka kumbe ndiyo kazi zake, nikampiga chini.

IJUMAA: Vipi kuhusu wewe na Fei Toto, ilikuwaje umtangazie ofa ya kukuoa bila mahari?

AGGY BABY: Kweli nilikuwa tayari kuolewa naye bila mahari, nampenda akiwa uwanjani, yeye ndiye aliyenifanifanya nihame Simba na kuhamia Yanga, ananifurahisha!
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz