Mke Amkata Mumewe Korodani Akidai Hazina Faida Kwani Hajawahi Mridhisha Kimapenzi Toka Waoane - EDUSPORTSTZ

Latest

Mke Amkata Mumewe Korodani Akidai Hazina Faida Kwani Hajawahi Mridhisha Kimapenzi Toka Waoane


Mwanaume mmoja nchini Kenya aitwaye Meme Kabati mwenye umri wa miaka 56 amelazwa Hospitali ya Nyambene Kaunti ya Meru baada ya Mkewe Karambu Meme, kumvuta na kuikata korodani yake moja kwa madai ya kwamba korodani hizo hazina faida kwakuwa Mumewe hajawahi kumridhisha kimapenzi kitandani hata siku moja wakati wanapofanya tendo la ndoa.

Tukio hilo limetokea wakiwa nyumbani kwao Igembe, Chifu wa eneo hilo la Ntunene aitwaye Edward Mutalii amesema alipata taarifa na alipofika eneo la tukio alikuta korodani ya Mwanaume huyo ikiwa chini baada ya kuvutwa sana mfuko wa uzazi na Mkewe na kuikata korodani moja.

Polisi wamemkamata Mwanamke huyo na kwa sasa anashikiliwa akisubiri kufikishwa Mahakamani lakini Mwanamke huyo anasisitiza amefanya hivyo kwakuwa kamwe Mumewe hajawahi kumridhisha wakati wa kufanya tendo la ndoa.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz