Msanii Mkongwe MB Dog Ampa Pole Harmonize "Anayopitia Konde Mimi Nimepitia Pia" - EDUSPORTSTZ

Latest

Msanii Mkongwe MB Dog Ampa Pole Harmonize "Anayopitia Konde Mimi Nimepitia Pia"

 

Ameandika MB Dog:

POLE RAJABU ABDUL KAHALI (KONDEBOY)

360 si mkataba mbaya kama unaelewa biashara ya muziki. Ukielewa terms na condition unatoboa but kwa mawazo yangu si mkataba mzuri kwa msanii underground ambae anaweza kuchipukia kupata nafasi na jina. Kwanza anakuwa hajakomaa kimuziki na hayuko tayari kupokea umaarufu na kuweza kujiongoza kwenye uhalisia wa kupambana na MAISHA.

NITAJITOLEA MFANO MIMI BINAFSI NILIANZA SAFARI YANGU YA MUZIKI MIAKA YA 2000 kwenda 2003 rasmi. Lakini nilipata umaarufu mkubwa nikiwa mdogo sana miaka 18 kwenda 20 ukomavu wangu kwenye biashara ya muziki na uelewa wangu ulikuwa mdogo sana hasa kujiongoza kuweza kubalance maisha binafsi na muziki pia umaarufu na watu walionizunguka.

Ilihitajika busara sana na uelewa mkubwa sana wa viongozi wangu ambao walinizunguka hasa msimamizi wa kampuni yetu kuniongoza kipindi hicho ambae kwa utendaji alikuwa Babu Tale, nilikuwa sijui chochote kuhusu kutunza pesa wala kutumia pesa. Nyimbo yangu ya kwanza LATIFA ndio ilikuwa chanzo kikuu cha mapato kwenye kampuni badala ya mimi kufanikiwa kurekodi kwa gharama za boss wangu r.i.p my boss ABDUL.

Ulinipa kila kitu bila maandishi ya aina yeyote mungu akulaze pema BONGE. Nilipata sifa zote kupitia roho yako na upendo wako kwa watu wote waliokuzunguka. Uliwaamini watu ambao pia walikuja kukuangusha na kutuangusha tuliokuzunguka na kuanza kutapatapa naamini ungekuepo mpaka leo usingekubali kuona mimi nashindwa kwa njia yeyote ile.

UNAYOPITIA KONDE MIMI NILISHAPITIA KUANZIA MIAKA YA 2007 MPAKA HIVI SASA 2021. NILIPOAMUA KUONDOKA KWENYE KAMPUNI ABDUL ALINIPA BARAKA LAKINI HAKUWA NA FURAHA SIKUELEWA SABABU NI NINI HASA. LAKINI NILIANZA KUJUA BAADA YA KUTOA NGOMA YANGU YA KWANZA MWAKA 2009 INAYOITWA NATAMANI. PESA ZILITOKA KUZUIA HII NYIMBO ISICHEZWE MEDIA ZOTE NA KIPINDI HICHO HAKUNA DIGITAL PLATFORMS YEYOTE HAPA BONGO.

NILIPAMBANA KUVUKA MIPAKA HATIMAE NGOMA IKARUDI BONGO NA KUNIPA HESHIMA YA MSANII BORA WA KIUME MWAKA 2009/2010. VIJANA SASA HIVI MNA NAFASI NYINGI UKIBANIWA RADIO UNAKWENDA YOUTUBE. SISI KIPINDI CHETU HAKUNA HIZO MITANDAO. KWA HIYO HAYA MAMBO YALIANZIA MBALI TOKA ENZI ZETU. BAADA YA KUTOA HIYO NGOMA MILANGO YA SHOW IKAANZA.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz