Maua Sama "Mpenzi Mzungu Alitaka Niache Muziki niwe Wife Material" - EDUSPORTSTZ

Latest

Maua Sama "Mpenzi Mzungu Alitaka Niache Muziki niwe Wife Material"
Kipindi cha nyuma habari zilikuwa nyingi kuhusu Maua Sama kutoka na Mzungu,na ikafika hatua hadi wakavalishana pete za uchumba na mzungu akashuka hadi Moshi kujitambulisha. Baadaye kidogo jini mkata kamba akapita na pete kidoleni ikavuliwa kuashiria,it's end over (kwa sauti ya Kinata Mc😁)

Sababu hasa za wawili hawa kubwagana hazikuwahi kujulikana,ila hii leo November 1,Mau Sama akiwa kwenye leo tena ya Clouds Fm amedai aliamua kutemana na mzungu sababu jamaa alitaka Maua aache muziki kisha aende ughaibuni kuwa wife material kitu ambacho Maua amedai ni maamuzi magumu ambayo hasingeweza kuyafanya hivyo akaona bora kuyabwaga tu.

@mauasama hii leo pia ameanzisha challenge ya Zai ambapo atayefanya clip bora kuliko wengine basi atajizawadia zawadi. Cha kufanya jirekodi video clip ukifanya matashititi ya Zai kisha post ukimtag naye bila hiyana atapitia.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz