Breaking News : Boardroom Lodge Yawaka Moto - EDUSPORTSTZ

Latest

Breaking News : Boardroom Lodge Yawaka Moto
MOTO mkubwa umezuka na kuunguza Boardroom Lodge (sehemu ya kulala wageni) iliyopo Sinza-Mapambano jijini Dar es Salaam, mchana huu wa leo, Novemba 1, 2021 huku chanzo cha moto huo kikiwa hakijajulikana.
Tayari kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kimefanikiwa kufika na kuudhibiti moto huo kwa kushirikiana na wasamaria wema waliokuwepo eneo la tukio.
Hata hivyo hakuna taarifa za majeruhi wala vifo vilivyosababishwa na moto huo huku tathmini ya madhara ikiwa haijafahamika.
Tukio hili linatokea ikiwa ni wiki moja tu tangu The Cask Bar iliyopo Rocky city Mall jijini Mwanza kuteketea usiku. Miezi mihache iliyopita, La Chaz Pub iliyopo Sinza Mori jijini Dar nayo iliteketea kwa moto.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz