Sio Masihara Drake Analipa Kodi ya Nyumba Mil. 500/- Kwa Mwezi - EDUSPORTSTZ

Latest

Sio Masihara Drake Analipa Kodi ya Nyumba Mil. 500/- Kwa MweziNYUMBA aliyokuwa anaishi staa wa muziki duniani, Drake, ambayo amehama hivi karibuni, haikuwa ya mchezo kwani kwa mwezi alikuwa analipa kodi ya Dola za Marekani 215,000 (takribani Sh mil. 500 za Tanzania).

Kwa mujibu wa jarida la New York Post, mzaliwa wa Canada huyo anayeishi Marekani analipa kiasi hicho kwenye mjengo wenye ukubwa wa meta za mraba zaidi ya 1672.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Drake aliposti nyumba hiyo hivi karibuni wakati akisherehekea ‘birthday’ yake ya kutimiza umri wa miaka 35.

Jamaa aliishi kwenye nyumba hiyo kwa wiki chache tu kwani hakuwa na mpango wa kuishi hapo muda mrefu kwa kuwa tayari ana mjengo mwingine wa maana nje ya Jiji la Los Angeles.


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz