Kutana na Mwanamke MREMBO Mwenye Ndevu Nyingi zaidi Kuliko Wanawake Wote Duniani "Nilishawahi Fikiria Kujiua" - EDUSPORTSTZ

Latest

Kutana na Mwanamke MREMBO Mwenye Ndevu Nyingi zaidi Kuliko Wanawake Wote Duniani "Nilishawahi Fikiria Kujiua"

Harnaam Kaur, mwanamke mwenye umri wa miaka 30 anayeishi katika Mji wa Slough, Kusini Mashariki mwa Uingereza ndiye mwanamke mwenye ndevu nyingi zaidi kuliko wote duniani.

Mrembo huyo ambaye ana tatizo la kuwa na vinyweleo vingi kupita kiasi, tatizo linalojulikana kitaalamu kama ‘polycystic ovary syndrome’, ameeleza kuwa alianza kupata tatizo hilo akiwa na umri wa miaka 11 na kwamba alikuwa akizinyoa mara mbili kwa wiki.

Alipokuwa shuleni alikuwa akionewa sana kwa kuitwa majina mengi ya kejeli kama ‘jike dume’, na kwamba alikuwa anashindwa hata kuwaangalia watu usoni na alipotoka shule alijifungia ndani siku zote asionekane mara kwa mara.

Pia ameongeza kwa kusema kutokana na kuishi katika hali hiyo alifikia hatua ya kufikiria kujiua.

Vilevile, Harnaam amesema kuwa amejiunga na dini ya Sikh na kubatizwa, ya kwamba imani ya dini hiyo hairuhusu watu kunyoa vinyweleo vyao kwa kuwa Mungu ndiye aliyewaumba hivyo. Kwa hiyo ameziachia nywele zake na sasa anaonekana kama mwanaume akiwa na nywele nyingi kidevuni, mikononi na kifuani.

Imani hiyo imempa ujasiri zaidi juu ya muonekano wake, na anajiona mwanamke mwenye mvuto zaidi.

Read More:Hatimaye Christina Shusho Afunguka Kuhusu VIDEO Inayoonyesha Akinywa Pombe na Wenzake


“Nahisi nimekuwa mwanamke zaidi, nina mvuto zaidi na nadhani naonekana hivyo pia. Nimejifunza kupenda jinsi nilivyo na hakuna kitakachonitikisa sasa hivi.” Alisema Harnaam.

Neno moja kwa mlimbwende huyu?

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz